
The United Republic of Tanzania
ARUSHA TECHNICAL COLLEGE
Skills make the difference

Post Details

PAC YAPONGEZA ATC KUMALIZA UJENZI KAMAPASI YA KIKULETWA
Kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Kampasi ya Kikuletwa iliyopo Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro, Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kwa matumizi mazuri ya fedha za umma yaliyopelekea kukamilisha ujenzi wa Kampasi hiyo. Akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kampasi hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Japhet Hasunga ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa ujenzi sambamba na kuona thamani halisi ya fedha ilyotumika. โNawapongeza sana kwa sababu mmefanya kazi nzuri sana, pili nampongeza rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya, alitupatia hizi fedha na Bunge liliidhinisha mpaka sasa vitu vinaonekana, kwa kweli kazi ni nzuri tunapongeza sana na thamani ya fedha kwa hatua mliyofikia inaanza kuonekanaโ alisema Mhe. Hasunga. Aidha Mhe. Hasunga ameiagiza Wizara ya Elimu Pamoja na Chuo hicho kuhakikisha Samani na vifaa vya Kufundishia vinapatikana haraka ili majengo hayo yaanze kutumika mara moja. โIsichukue muda mrefu Samani, mitambo na vifaa vingine vya kufundishia vipatikane, majengo haya yakikaa muda mrefu yataanza kuchakaaโ aliongeza Mhe. Hasunga. Katika hatua nyingine Kamati hiyo ya PAC ilitembelea ujenzi wa mtambo wa kufua Umeme kinachojengwa Chuoni hapo ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia 20% na inatarajiwa baada ya kukamilika kitazalisha Megawati 1.65 ambazo zitaunganishwa kwenye gridi kuu ya Taifa. Kampasi ya Kikuletwa imejengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa Afrika Mashariki wa kujenga ujuzi kwa mlingano na uingiliano wa Kikanda (EASTRIP) ambao umetoa jumla ya shilingi bilioni 37 za Tanzania kuiboresha Kampasi hiyo kuwa kituo cha Umahiri kwenye sekta ya nishati jadidifu.
Other Posts