+255-(0)27- 297 0056 Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads rector@atc.ac.tz SMS Online Application CMU

contact info

+255-(0)27- 297 0056
Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads
SMS
CMU

Post Details

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EASTRIP ATC

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EASTRIP ATC Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Tarehe 21/10/2023 ilitembelea Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kampasi ya Kikuletwa na kukagua mradi wa kujenga ujuzi na ushirikiano Afrika Mashariki (EASTRIP) pamoja na kupokea taarifa ya Maendeleo ya mradi. Kamati hiyo ilipokelewa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar J. Kipanga na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Musa N. Chacha, ambao kwa pamoja walitembelea mradi unaoendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa majengo ya madarasa, karakana, mabweni Pamoja na Ukumbi wa Mihadhara inayofadhili na serikali kupitia Benki ya Dunia. Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezi, Mhe. Husna Juma Sekiboko, amepongeza jitihada kubwa za uongozi wa Chuo katika utekelezaji wa Mradi na kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Elimu, kuangalia namna bora ya kuongezea nguvu kwenye mradi huo ili ukamilike kwa wakati. ‘’ Kimsingi tumetembelea maeno mengi tumejionea wenyewe kile ambacho mnatekeleza kwenye Chuo hiki. Niwapongeze mradi unatekelezwa Pamoja na changamoto nyingi ambazo tulielezwa kwenye kikao tukiwa Dodoma na hata tulipofika hapa kunachangamoto nyingi ambazo zimesababisha mradi kuchelewa lakini kifupi mnafanya vizuri, viwango ni vizuri, tunaridhika na utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri’’ alisisitiza Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omar J. Kipanga, ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea Chuo cha Ufundi Arusha, Kampasi ya Kikuletwa, na kuahidi Wizara itatekeleza maoni., ushauri, mapendekezo na maagizo yote ya kamati ili kufanyia kazi na kuboresha huduma zitakazo tolewa na chuo cha Ufundi Arusha. Akiwasilisha taarifa ya Chuo kwa Kamati, Mkuu wa Chuo Dkt. Musa Chacha amesema, utekezaji wa mradi huo umefikia asimilia 62

  Oct 24, 2023   |