+255-(0)27- 297 0056 Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads rector@atc.ac.tz SMS Online Application CMU

contact info

+255-(0)27- 297 0056
Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads
SMS
CMU

Post Details

WIZARA YA ELIMU YARIDHISHWA NA BUNIFU ZA WANAFUNZI CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC)

Wiki ya ubunifu, utafiti na ujasiriamali Chuo cha ufundi Arusha imehitimishwa leo tarehe 23 05.2025 ambapo bunifu zenye malengo ya kutatua changamoto kwenye sekta mbalimbali zimeonekana. Akihitimisha wiki hiyo ya ubunifu Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi kutoka wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia Dkt. Fredrick Salukele ameonesha kuridhishwa na bunifu za wanafunzi hao kutoka ngazi mbalimbali ikiwemo sekta ya madini, viwatilifu, maabara, Tehama,na utalii. โ€œNawapongeza wabunifu wote kwa kazi zenu nzuri, watu wengi wanafikiri ubunifu ni kuanzisha kitu kipya, Hapana hata kuendeleza kile kilichopo kwa namna tofauti ni ubunifu pia, ninawapongeza sana kwa hatua hiiโ€ alisema Dkt. Salukele. Aidha Dkt. Salukele aliwataka wabunifu wote kuzitangaza bunifu zao kwenye vyombo mbalimbali vya Habari ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo vijana wengi wanafuatilia taarifa huko, hiyo itasaidia bunifu hizo kuonekana na kuendelezwa, Kwa upande wake mkuu wa chuo Cha Ufundi Arusha Profesa Musa Chacha amesema โ€œTutazipitia bunifu zote za wanafunzi wetu, hata wale ambao hawakushinda kwenye mashindano haya tutaangalia bunifu zao kama zinaweza kutatua changamoto kwenye jamii tutaziendelezaโ€ alisema Prof. Chacha. Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Wiki hiyo ya Ubunifu, Utafiti na Ujasiriamali, Dkt Josephat sengura amesema wiki hiyo ilianza tarehe 19 hadi 23 Mei 2025, iliwezesha wanafunzi hao kupata fursa ya kuonesha mawazo ya kibiashara, kukutana na wataalamu kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Usajili wa Biashara (BRELA) ili kupata elimu ya kuweka Mawazo yao katika misingi Bora ya kibiashara.

  May 29, 2025   |     Download

Other Posts