+255-(0)27- 297 0056 Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads rector@atc.ac.tz SMS Online Application CMU

contact info

+255-(0)27- 297 0056
Junction of Moshi-Arusha and Nairobi Roads
SMS

Post Details

ATC Yaadhimisha Msimu wa Tatu wa Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Ujasiriamali

ATC Yaadhimisha Msimu wa Tatu wa Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Ujasiriamali -Kukuza Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Shigeki Komatsubara, amesema uwekezaji katika ubunifu, utafiti na ujasiriamali wa vijana ni nguzo muhimu katika kuharakisha maendeleo endelevu ya taifa. Bw. Komatsubara amesema hayo Juni 15 ,2026 wakati akifungua Msimu wa Tatu wa Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Ujasiriamali katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unaofanyika kuanzia Juni 15 hadi 19, 2026. Ameongeza kwa kueleza kuwa UNDP itaendelea kuunga mkono ubunifu, maendeleo ya kidijitali na ujasiriamali wa vijana ili kuwasaidia kubadili mawazo yao kuwa suluhisho na biashara zenye tija. Huku akipongeza kiwango cha ubunifu kilichooneshwa na wanafunzi wa ATC, ambapo bunifu nyingi zimeonyesha uwezo wa kutatua changamoto halisi zinazoikabili jamii na kuchangia maendeleo ya kiuchumi. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Prof. Mussa Chacha, amesema ushiriki wa wanafunzi waliomaliza ATC katika maadhimisho hayo unalenga kuwahamasisha wanafunzi waliopo chuoni kuendelea kuamini katika ndoto zao, kutumia maarifa waliyojifunza kujiajiri na kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii. Amesema chuo hicho kimeendelea kuibua na kuendeleza mawazo bunifu yenye uwezo wa kutekelezeka, akitolea mfano mradi wa mita janja za maji zinazolipiwa kabla ya matumizi (Water Prepaid Meter) ulioanzishwa chuoni hapo na kufikia hatua ya kutumiwa na mamlaka mbalimbali za maji nchini baada ya kuendelezwa kwa msaada wa kitaalamu na kifedha. Prof. Chacha ameongeza kuwa chuo kinaendelea na Ujenzi wa Kiwanda cha Mafunzo na Uzalishaji (Industrial Workshop) kitakachokuwa kitovu cha kuzalisha na kuendeleza bunifu za wanafunzi, huku maadhimisho ya wiki hiyo yakitarajiwa kuendelea hadi Juni 19 kwa maonesho ya teknolojia, mijadala ya kitaalamu na shughuli za ujasiriamali zinazolenga kukuza ubunifu na maendeleo kwa vijana.

  Jun 15, 2026   |