The United Republic of Tanzania
ARUSHA TECHNICAL COLLEGE
Skills make the difference
Post Details
ATC, RUWASA WAINGIA MAKUBALIANO YA KUTENGENEZA MITA JANJA ZA MAJI ZA MALIPO YA KABLA
Chuo cha ufundi Arusha (ATC) kimesaini hati ya makubaliano na Ruwasa kuhusu uzalishaji wa mita janja ambazo zinaruhusu malipo kabla ya matumizi ya huduma za maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais. Akizungumza mara baada ya kusaini hati hiyo Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha ,Profesa Mussa Chacha amesema kuwa , chuo cha ufundi Arusha kina majukumu matatu ikiwemo kufundisha ,kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu ambapo hili eneo la utafiti ndilo hasa limewafanya kuwa na mahusiano na Ruwasa . Amesema kuwa ,Ruwasa walikuwa na changamoto ya kiutendaji ambapo walitaka wananchi wapate mita janja (smart Meter ) ambapo waliingia makubaliano ya kuanza kufanya utafiti wa miaka mitatu kwa pamoja ambapo mwishoni waliweza kupata mita ambazo zinafaa na zilizoboreshwa . Ameongeza kuwa, tayari wananchi wana uelewa kuhusu mita hizo na kuna wananchi ambao tayari wanazitumia ambapo wamegundua kuwa zinafanya kazi vizuri kwa mazingira ya kitanzania na ndio maana leo wakafikia hatua ya kuingia makubaliano na Ruwasa kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa hizo mita kwa wingi . โSisi chuo cha ufundi Arusha tunawahakikishia Ruwasa kuwa Teknolojia tunayo na wameshaidhibitisha na uwezo wa kuzalisha pia tunao na ukiangalia chuo cha ufundi Arusha tuna wanafunzi zaidi ya 5,000 hapo chuoni hivyo kiwanda hicho licha ya kwamba kinatumika kwenye uzalishaji bali ni sehemu ya mafunzo kwa wanafunzi wao ambapo hata wataalamu wanaojua teknolojia hiyo watawaajiri baadaye .โamesema Prof Chacha . Ameongeza kuwa ,mita hizo zinatengenezwa na watanzania kwa maana ya wataalamu wa ndani ambao pia wametengeneza mfumo mzima wa hizo mita ambapo hata matengenezo yale wataalamu wa ndani ndo watakuwa wanafanya na zoezi hili ni endelevu . โKupitia hizi mita tutaweza kuharakisha maendeleo ya watanzania kwani wanaotengeneza ni watanzania na vijana watapata ajira kupitia uzalishaji huo kwani mchakato huo umekuwa ni jumuishi na utasukuma maendeleo ya watanzania.โamesema Profesa Chacha . Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA ,Injinia Wolta Kirita amesema kuwa uwekaji wa mita ni sehemu ya uwekezaji ambapo mita hizo zitafungwa kwa gharama za Ruwasa na kwa zile gharama ambazo wananchi wamechangi
Other Posts