
The United Republic of Tanzania
ARUSHA TECHNICAL COLLEGE
Skills make the difference

Post Details

ššš ššššššš ššššššš šš ššššššššššš šš šššššš ššš ššššš šš šššššš
Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kupitia Kampasi ya Kikuletwa kiko mbioni kujenga kituo cha kufua umeme kwa njia ya maji kitakachotumika kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa Kampasi hiyo Pamoja na kuunganishwa kwenye gridi ya taifa. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Chuo hicho kupokea eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 100 lililopo katika Kijiji cha Kambi ya Chokaa kilichopo Kata ya Naisinyai Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara ambapo uongozi wa Kijiji hicho umeridhia kutoa ardhi hiyo kwa Chuo cha Ufundi Arusha. Katika hafla ya utiaji Saini makubaliano ya mkataba wa kupokea ardhi hiyo iliyofanyika Chuo cha Ufundi Arusha, Mkuu wa Chuo hicho Prof. Musa Chacha ameeleza baadhi ya faida zitakazopatikana baada ya kuanza uwekezaji kwenye ardhi hiyo ikiwa ni Pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya kwenye Kijiji hicho cha Kambi ya Chokaa kitakachotoa huduma kwa wanakijiji wote. Vilevile Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kuanza shughuli za uzalishaji umeme kwenye ardhi hiyo kitakua kinatoa sehemu ya faida inayopatikana kutokana na uzalishaji huo kama mchango kwa jamii. Aidha Chuo kitakua kinatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi watano (05) wa kijiji cha Kambi ya Chokaa watakao kua na sifa ya kujiunga na kozi mbali mbali zinazotolewa kwenye Kampasi yake ya Kikuletwa kila mwaka tangu tarehe ya kusainiwa kwa makubaliano ya mkataba huo. Kwa kuhitimisha, Chuo kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji cha Kambi ya Chokaa, watazijengea uwezo maabara za sayansi zilizopo shule ya sekondari iliyopo kambi ya Chokaa kwa lengo la kuwaanda wanafunzi katika masomo ya sayansi.
Other Posts