ARUSHA TECHNICAL COLLEGE
TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTIONS TRADE UNION (THTU)
TANZANIA HIGHER LEARNING INSTITUTIONS TRADE UNION – THTU, WAS REGISTERED UNDER SECTION 48 (5) OF EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, No. 6 of 2004 AND ISSUED UNDER SECTION 43 (2) OF THE LABOUR INSTITUTIONS ACT, No. 7 of 2004 DATED 12TH DAY OF DECEMBER, 2008, AT DAR ES SALAAM.
VIONGOZI WA CHAMA NGAZI YA TAWI
Castory Mkumba Mwenyekiti |
Sospeter Iman Katibu
|
Mweka Hazina |
Isabela R. Lyimo Mratibu Mkuu Wanawake |
Imelda Mdaba Mratibu Msaidizi Wanawake |
Godson E. Mushi Mwakilishi Taifa
|
WAJUMBE WA BARAZA
Ambrose C |
Spatro N |
Elisante Tembe |
Mary Senya |
Theclah Mng'anya
|
Timothy Meshack |
Dotto J |
Yohana Kiyovelwa |
Kastuli J |
|
MADHUMUNI YA THTU
Dhumuni kuu la THTU ni kusimamia kwa vitendo ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi. Madhumuni mengine ni pamoja na;
1.Kutetea maslahi ya wafanyakazi
2.Kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa wafanyakazi na Menejimenti ili kuleta tija
USHIRIKISHWAJI.
Kuna aina zifuatazo za ushirikishwaji wa Wafanyakazi Chuo cha Ufundi Arusha;
1.Baraza la Wafanyakazi (Workers Council).
Hili linaundwa na Chama cha THTU na Menejimenti ya Chuo. Lengo kuu la Baraza hili ni Kupitia Bajeti, sera na Mipango ya Maendeleo ya Chuo na kuishauri Menejimenti namna bora ya kutekeleza.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
Kaimu MwenyeKiti THTU Taifa (Dr. Emelia Mgozigwa) Katika Mkutano na Wajumbe wa Halmashauri ya THTU-ATC.
2.Majadiliano ya pamoja na kufunga Mkataba wa Hali Bora (Collective Bargaining Agreements).
THTU inawakilisha wafanyakazi wote katika majadiliano ya pamoja na Menejimenti katika masuala yote yanayohusu maslahi,mahusiano na maendeleo ya wafanyakazi na Taasisi kwa ujumla. Katika kutekeleza hili THTU imeandaa Mkataba wa hali bora za wafanyakazi ambao utatekelezwa baada ya kuridhiwa na Baraza na kusainiwa na THTU, Menejimenti na Msajili wa Hazina.
3.Mikutano ya Kikatiba ya Wanachama
THTU ina mikutano ya wanachama ya kikatiba, yenye lengo la kushirikisha wafanyakazi kuzungumza na kutoa maoni, ushauri na mapendekezo ya kutekeleza uboreshaji wa maslahi, mazingira ya kazi na mahusino mazuri kazini.
4.Shere za Wafanyakazi Mei Mosi
THTU kwa Kushirikiana na chama mwenza cha Wafanyakazi cha Researchers, Academicians and Allied Workers Union- RAAWU, Huandaa kwa ushirikiano maazimisho ya sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi.
Wafanyakazi wa ATC wakifurahia kwa pamoja
Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani,
Mei Mosi 2017 Mmoja wa Wafanyakazi Hodari ATC 2017; PrayGod Lameck
(Koti Jeusi), akifurahia Mei Mosi na Wafanyakazi wenzake
SHABAHA YA USHIRIKISHWAJI
Shabaha za kimsingi za Ushirikishwaji ni kama ifuatavyo:-
i. Kupunguza matumizi mabaya ya madaraka yanayotokana na utaratibu wa umilikaji wa njia kuu za uchumi.
ii. Kujenga jamii isiyokuwa na matabaka na kumwezesha mfanyakazi kushiriki katika kutunga sera na mipango ya uchumi kitaifa
iii. Kujenga jamii ambayo haina tabaka na kwamba umilikaji na uendeshaji wa njia kuu za uchumi ni wa pamoja.
iv. Kuleta uhusiano na ushirikiano mwema mahali pa kazi kwa lengo la kuinua ufanisi wa kazi.
v. Kudumisha demokrasia mahali pa kazi, viwandani, mashirika ambapo wafanyakazi wataweza kujadiliana pamoja.
vi. Mambo muhimu katika demokrasia ni kama ifuatavyo
• Uhuru na majadiliano.
• Uhuru wa kufikia uamuzi
• Utekelezaji wa pamoja wa maamuzi hayo (Binding to all).
• Wafanyakazi wenyewe wataweza kuongeza juhudi na maarifa kazini, na pia watazidi moyo wa uvumbuzi, utundu, ubunifu katika utengenezaji wa vitu vipya.
Viii. Wafanyakazi watakuwa tayari kukubali madaraka makubwa zaidi katika uendeshaji wa Taasisi.
Ix Kupunguza migogoro mahali pa kazi.
X Kuwawezesha wafanyakazi na Menejimenti kuwa na msimamo wa pamoja(mshikamamo) kuhusu masuala yanayohusu kazi na ustawi wa wafanyakazi.
Xi Kuleta ufanisi na tija mahali pa kazi
Xii Kuwawezesha kutumia vipaji vya wafanyakazi ipasavyo
Umuhimu wa Ushirikishwaji (Ushirikishwaji kupitia Agizo la Rais Na. 1 la 1970)
Kuwa na utawala bora mahali pa kazi kwa kutimiza misingi ifuatayo:-
• Uwajibikaji
• Uwazi
• Utawala wa Sheria
• Ushirikishwaji
• Uwiano sawa
• Mrejesho (haraka na chanya)
• Ufanisi
• Maafikano
Sheria zifuatazo zinaimarisha na zinalinda Dhana hii ya ushirikishwaji:-
• Mkataba wa ILO wa Philadephia 1944
• ILO convention No. 98 of 1948
• Agiza la Rais Na. 1 la 1970
• Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 (Uhuru wa kutoa mawazo)
• Sheria ya Majadiliano Katika Majadiliano Katika Utumishi wa Umma Na. 19 na Kanuni za 2005.
• Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 za 2002 na Kanuni za 2003.
• Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya2004
• Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya 2004.
• Mikataba ya kuunda baraza
• ILO Recommendation No. 129 of 1967 (communications within undertaking).
• Equal Remuneration convention No. 100 of 1951